Leverage katika forex - jinsi ya kuitumia kwa busara

Michael Stark

Kiongozi wa Maudhui ya Kifedha wa Exness

Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.

Shiriki

Leverage katika forex na CFDs zingine ni huduma inayotolewa na brokers. Kwa kawaida inakuruhusu kufanya trade zaidi, kwa kutumia kiasi kile kile cha pesa kwenye akaunti yako ya kutrade. Matumizi ya leverage ni tofauti kuu kati ya kutrade CFDs, ambazo ni bidhaa zinazotokana na mali zingine, na kutrade mali zinazoweza na mali zingine.

Makala haya yanajibu maswali yoyote uliyo nayo kuhusu leverage katika forex na inaelezea maana yake kwako kama trader. Endelea kusoma ili kuelewa jinsi leverage hufanya kazi na maelezo ambayo unapaswa kujua kabla ya kutrade kwa kutumia leverage ya juu.

Je, leverage ni nini katika biashara ya forex?

Leverage ni huduma unayoweza kutumia kufungua orders kubwa zaidi ya zile ambazo ungeweza kwa kutumia funds ulizoweka kwenye akaunti yako pekee. Leverage sio mkopo bali ni uwiano wa funds zako halisi kwa kiasi unachoweza kutrade kwa kutumia leverage.

Kiasi cha leverage unachoweza kutumia kufungua positions kinategemea mambo kadhaa, kama vile instrument unayofanyia biashara, habari muhimu za soko la forex na salio lako. Kabla ya kuangazia mambo haya kwa kina, hebu tuchunguze mambo muhimu ya jinsi leverage inavyofanya kazi.

Mambo muhimu ya leverage

Ikiwa wewe ni trader anayetumia leverage ya 1:100, inamaanisha kuwa kwa kila dola unayoweka, unaweza kufanya trade kana kwamba una dola 100 kwenye akaunti yako ya kutrade. Hiyo huathiri margin, kiasi cha mtaji kinachohitajika ili kufungua trade na kuiweka ikiwa imefunguliwa.

Unapotumia leverage, masharti yako ya margin huwa chini. Hivi ndivyo unavyoweza kuikokotoa:

contract size*ukubwa wa lot/leverage = margin inayohitajika

Kukokotoa margins kwa kutumia leverage

Hebu tuone jinsi ya ukokotoaji wa leverage ya forex unavyofanya kazi ikiwa ungependa kununua lots 0.2 za dola-yen (USDJPY) kwa leverage ya 1:500:

Margin ya 0.2 ya USDJPY, leverage 1:500: 100,000*0.2/500 = $40

Iwapo unatumia leverage ya 1:500, utahitaji $40 kama margin kwa lots 0.2 za USDJPY. Bila leverage, utahitaji margin ya $20,000.

Kumbuka kuwa hauitaji kukokotoa margins wewe mwenyewe bila kujali leverage unayotumia. Badala yake, unaweza kutumia Kikokotoo cha Uwekezaji cha Exness.

Uhusiano kati ya leverage, margin na zaidi

Leverage ni moja wapo ya sababu kuu zinazoathiri nambari unazoona kwenye jukwaa. Haya hapa ni maelezo yake:

  • Salio ni pesa halisi ulizo nayo kwenye akaunti yako.
  • Equity ni salio lako pamoja na au ikiondolewa faida au hasara yoyote inayopatikana. Ikiwa huna positions zozote zilizofunguliwa, equity na salio lako zitakuwa sawa.
  • Margin ya Forex au margin iliyotumika ni kiasi cha pesa ukiondoa funds zenye leverage zinazohitajika kuweka trade ikiwa imefunguliwa.
  • Jumla ya margin au margin iliyotumika ni margin iliyounganishwa ya positions zako zote. Inaweza pia kuitwa ‘margin’ ikiwa muktadha uko dhahiri au hauhitajiki kuwa mahususi.
  • Free margin ni kiasi cha pesa ulicho nacho ili kufungua orders mpya.
  • Margin level ni asilimia ya equity yako ikilinganishwa na jumla ya margin yako.
  • Kisanduku cha zana katika MT5 huonyesha takwimu hizi zote pamoja katika sehemu moja.

    Katika mfano huu kutoka MT5, trader ana position ndogo ya dhahabu na leverage ya 1:100. Kumbuka kuwa jukwaa la wavuti la Exness, MT5, au jukwaa lolote unalotumia kwenye kifaa chochote hukusaidia kujifunza kuhusu leverage na margin. Majukwaa haya hukokotoa equity, margin, free margin na margin level kiotomatiki, kwa hivyo hauhitajiki kufanya hivyo wewe mwenyewe.

    Kutumia leverage

    Mara tu unapoelewa misingi ya jinsi leverage hufanya kazi, unagundua kuwa inatoa fursa kubwa na changamoto kubwa katika biashara. Unahitaji kiwango fulani cha leverage ili kutrade kwa kuwa huenda hungependa kuweka pesa nyingi.

    Kutumia leverage katika biashara

    Leverage ina uwezo wa kuongeza faida zako lakini pia hasara zako. Hii ni kwa sababu kufanya biashara ya viwango vya juu huongeza utendaji, uwe mzuri au mbaya. Traders wasio na ujuzi na wasio makini mara nyingi hupoteza pesa nyingi zaidi ya traders wa forex wenye uzoefu.

    Hakuna leverage iliyo sahihi kabisa kwa kila trader. Inategemea malengo yako, uzoefu, hali ya kifedha na mambo mengine. Kwa maelezo hayo, unaweza kujaribu viwango tofauti vya leverage na salio tofauti kwa kufanya mazoezi ukitumia akaunti ya demo bila malipo.

    Leverage katika Exness

    Exness hutoa leverage isiyobadilika na inayobadilika kulingana na instrument. Instruments ambazo zina leverage isiyobadilika ni pamoja na cryptocurrencies, ilhali zile zilizo na leverage inayobadilika ni pamoja na forex na zingine nyingi.

    Leverage yako ya juu zaidi inayopatikana hupungua kadiri salio lako linapoongezeka. Kwa mfano, ikiwa salio lako linazidi $1,000 (au kiwango sawa katika sarafu nyingine) huwezi kutumia Leverage Isio na Kikomo. Hata hivyo, unaweza kutoa pesa au kufungua akaunti nyingine ili kutumia Leverage Isio na Kikomo.

    Leverage yako ya forex pia huwekewa vikwazo wakati wa habari kuu. Dakika 15 kabla hadi dakika 5 baada ya matoleo makubwa kama vile ripoti ya ajira ya Marekani (pia inajulikana kama ‘NFP’), leverage ya juu zaidi ya positions mpya ni 1:200 kwa instruments nyingi au 1:50 kwa indices.

    Kunaweza kuwa na hali zingine nadra ambapo leverage ya juu zaidi inayopatikana ni ndogo kuliko ile ambayo ungependa kutumia. Unaweza kufikia taarifa zaidi kupitia Kituo chetu cha Usaidizi kupitia Eneo lako la Kibinafsi mara tu unaposajili akaunti katika Exness.

    Kuchagua kiwango cha leverage ambacho ungependa kutumia

    Ili kubadilisha leverage kwa akaunti yako yoyote, anza kwa kuingia kwenye Eneo la Binafsi la Exness. Kwenye ukurasa mkuu wa Eneo la Binafsi, ‘Akaunti Zangu’, pata akaunti ambayo ungependa kubadilisha leverage na ubofye nukta tatu zilizo upande wa kulia wa kitufe cha manjano. Kisha bofya 'Badilisha leverage ya juu zaidi' na utaona skrini hii.

    Hapa ndipo unaweza kubadilisha leverage ya juu zaidi katika Eneo lako la Binafsi katika Exness.

    Kwenye menyu kunjuzi, chagua leverage unayopendelea na itabadilika. Hata hivyo, kumbuka kuwa, kama ilivyoelezwa hapo juu, ukichagua leverage ya juu, hii haitawezekana kila wakati, kama ilivyoelezewa kwenye taarifa katika skrini hii:

    Ni muhimu sana kusoma madokezo haya kwa uangalifu unapobadilisha leverage yako.

    Je, leverage huongeza hatari na kusababisha hasara?

    Jibu rahisi ni ‘hapana’. Biashara mbaya na ya kiholela husababisha hasara na huongeza hatari. Kuna sababu nyingi zinazosababisha hasara: matarajio yasiyoweza kufikiwa na ulafi, uwekaji mbaya wa viwango vya kusitishwa na malengo, uvivu katika kutafiti na kufuatilia trades.

    Hatari na leverage

    Leverage haisababishi hasara moja kwa moja au kuongeza hatari: hata hivyo, kunaweza kuongeza ukubwa wa hasara au faida zako.

    Hebu tuchukulie kuwa unatumia leverage ya 1:20 na uuze lot 0.01 ya euro-dollar (EURUSD). Kwa bahati mbaya, trade yako isababishe hasara ya pips 20, kwa hivyo utapoteza $2.

    Ikiwa ungekuwa unatumia leverage ya 1:2000 badala yake na ukatumia kufanya trade ya lot kamili badala ya lot 0.01, matokeo yangekuwa makubwa zaidi. Utapoteza $200 badala ya $2. Leverage inaweza sababisha hasara kuwa kubwa zaidi kuliko jinsi ingekuwa bila leverage, lakini haisababishi hasara.

    Faida zinazoweza kutokea kwa kutumia leverage

    Ikiwa wewe ni trader mzuri, leverage inaweza kuongeza faida zako. Kama ilivyoelezwa hapo juu, kiasi fulani cha leverage ni muhimu ili kufikia masharti ya margin kwa trades kubwa na kufanya biashara kuwa na thamani.

    Hebu fikiria kuwa unafungua orders 100 ndani ya kila miezi mitatu na, bila leverage, kila trade ina thamani ya $2. Ukipata faida ya 60% kwa wakati huo, faida ya jumla ya $120 ukiondoa hasara ya jumla ya $80, hii italeta faida yako ya kila robo mwaka kuwa $40 pekee. Kwa mtu wa kawaida, thamani yake ni ndogo.

    Faida na hasara kwa kutumia leverage

    Kwa upande mwingine, ikiwa ungetumia leverage ya 1:100, faida yako ya kila robo mwaka katika hali hiyo itakuwa $4,000. Hata hivyo, kumbuka kuwa ikiwa uwiano wa faida na hasara ungebadilishwa, leverage ya 1:100 ingemaanisha hasara ya kila robo ya $4,000.

    Jambo la msingi ni kwamba traders wenye ujuzi na waliofanikiwa hawapaswi kuwa na hofu ya kutumia leverage kwa kuwajibika. Leverage ni moja wapo ya sababu kuu zinazofanya trade ya CFDs kuwa ya thamani kwa trader wa aina hii.

    Vidokezo vinavyoweza kutumika vya kufanya biashara kwa kutumia leverage

    Ingawa kuna tofauti nyingi kati ya kubahatisha kwenye CFDs na kuwekeza katika mali zinazotokana na mali nyingine, leverage ndiyo inaonekana kuwa na manufaa zaidi. Unaweza kudhibiti kiasi kikubwa cha pesa na kuweka kiasi kidogo, ambayo inafanya iwe rahisi kupoteza pesa nyingi haraka, na unahitaji kuepuka hilo. Licha ya kuelewa leverage ya forex sharti pia ujue jinsi ya kuitumia.

    Kujifunza jinsi ya kufanya biashara sio mashindano

    Fikiria kuhusu ujuzi mwingine wowote ambao umejifunza kando na biashara. Ulipojifunza kuendesha gari kwa mara ya kwanza, je, ulianza na Maserati au Tesla? Ikiwa umekamilisha huduma ya kijeshi, je, silaha nzito ndiyo ilikuwa silaha ya kwanza uliyofyatua? Je, casoulet ndicho chakula cha kwanza ulichopika.

    Hapana. Ni sawa na biashara: usianze na leverage ya 1:2000. Jaribu viwango vya chini kwanza na uongeze kadri maarifa na ujuzi wako unavyoongezeka.

    Angalia kabla ya kuruka

    Takriban kila trader mwenye uzoefu alipata stop out kwa pesa alizoweka kwa mara ya kwanza. Mtu yeyote anayesema vinginevyo ana nidhamu kubwa sana ya kibinafsi na amebobea katika kudhibiti hatari, au hasemi ukweli.

    Watu wengi huanza biashara ya forex na akaunti za moja kwa moja zenye leverage kabla ya kuwa tayari. Iwapo huna uhakika kuhusu utayari wako, tumia muda mwingi kufanya mazoezi kwenye akaunti ya demo na kutafiti zana kuu za kudhibiti hatari. Hii haimaanishi kuwa unahitaji kutumia akaunti ya demo kwa miaka mingi, tumia tu kwa wakati wa kutosha kufanya mazoezi katika hali mbalimbali kulingana na jinsi ungefanya katika hali halisi kabla ya kuweka pesa halisi.

    Kuwa na kanuni zilizojaribiwa na uzifuate

    Kama trader wa rejareja au wa kitaaluma, unaweza kuwa na kanuni kali kuhusu kupungua kwa thamana na margin level. Ukifuata kanuni hizi kwa sababu umezijaribu na kugundua kuwa zinasaidia kupunguza hatari ya kifedha na kihisia. Huu ni mkakati mzuri wa kutumia ikiwa wewe ni trader mpya.

    Kwa mfano, unaweza kuweka kanuni ya kutofungua positions zozote mpya ikiwa margin level yako itashuka chini ya 200%. Hii inakupa nafasi kwa hasara yoyote kubadilika na kuwa faida, ikizingatiwa kuwa mawazo asilia ya trades yalikuwa sawa. Mbinu hii pia hupunguza shinikizo la kufunga trades zinazopata hasara mara moja.

    Maswali yanayoulizwa sana

    Leverage nzuri ya kuomba katika masoko ya forex au CFDs nyingine inategemea udhibiti wako wa hatari na nidhamu. Hakuna jibu sahihi kwa swali hili.

    Kabla ya mabadiliko ya udhibiti mnamo 2018, brokers wa Ulaya walitumia 1:200 kama leverage ya kawaida. Traders wengi bado hutumia hii. Ni nambari rahisi ambayo hukurahisishia kuhesabu margins kichwani mwako. Inatoa options nyingi kwa kiasi kidogo cha pesa kilichowekwa lakini haiko juu sana kwamba hatari ya kufanya biashara ya kupita kiasi inakuwa juu sana.

    Baadhi ya traders wanapendelea kutumia leverage ya chini, hasa ikiwa wameweka kiasi kikubwa cha pesa. Wengine wanapendelea leverage ya juu. Inategemea mapendeleo yako, lakini zingatia ujuzi wako kabla ya kuchagua 1:2000 au Leverage Isiyo na Kikomo. Ikiwa hupati faida mara kwa mara katika trades zako, kutumia leverage ya juu kunaweza kusababisha hasara kubwa.

    Ili kukokotoa leverage katika forex, chukua nambari ya pili katika uwiano wa leverage, kama 100 katika 1:100. Unaweza kuizidisha kwa salio lako au uitumie kugawanya margin isiyo na leverage, kulingana na kile ambacho ungependa kukokotoa.

    Kwa mfano, ikiwa ungependa kukokotoa margin ya forex inayohitajika ili kufanya trade kwa kutumia kiasi cha pesa ulichoweka cha $200 na kutumia leverage ya 1:2000, ungezidisha 200 kwa 2,000. Hiyo inakupa $400,000.

    Iwapo ungependa kukokotoa margin ya forex inayohitajika kwa nusu ya lot (lot 0.5) ya euro-dollar na leverage ya 1:50, ungegawanya 50,000 kwa 50. Hiyo inakupa €1,000.

    Unaweza kupata maelezo ya jinsi ukokotoaji inavyofanya kazi chini ya sehemu iliyo hapo juu, ‘Kukokotoa margins kwa kutumia leverage’. Hata hivyo, huna haja ya kufanya ukokotoaji wewe mwenyewe: jukwaa lako unalopendelea na kikokotoo cha traders cha Exness kinaweza kukufanyia.

    Mbinu bora zaidi kwa traders wageni katika kufanya biashara ya CFDs ni kuweka leverage kuwa chini zaidi iwezekanavyo. Unahitaji leverage fulani ili kufanya CFDs ziwe na faida nzuri, ndiyo, lakini unahitaji kuunda mkakati thabiti na uangalie matokeo kwanza kabla ya kuongeza hadi leverage ya juu.

    Unaweza kufanya mazoezi kwa urahisi kwenye akaunti ya demo katika Exness kwa kutumia viwango tofauti vya leverage. Jaribu mbinu zako chini ya masharti yanayokaribiana na hali halisi iwezekanavyo na utathmini kile kinachoenda vizuri na unachohitaji kubadilisha.

    Fanya mazoezi kwa wiki chache kwanza kabla ya kuanza biashara halisi kwa kutumia leverage. Anza na leverage ya chini zaidi inayopatikana katika Exness, ambayo ni 1:2. Ikiwa unapata faida mara kwa mara, unaweza kufikiria kuhusu kuongeza leverage yako baadaye.

    Kutrade kwa kutumia leverage: zingatia ujuzi wako

    Kwa kutumia au kutotumia leverage, biashara ni hatari. Shughuli za kifedha zilizo na uwezekano wa mapato ya juu pia huja na hatari kubwa. Ukifanya trade kwa kutumia leverage juu na usidhibiti hatari, kuna uwezekano wa kupoteza pesa nyingi. Hata bila leverage, ikiwa hukudhibiti hatari, bado unaweza kupoteza pesa, lakini ndogo.

    Je, wewe ni trader mzuri? Ukisema 'hapana', pengine ni jambo la busara kuweka leverage yako kuwa chini iwezekanavyo ikiwa utachagua kufanya trade halisi. Jambo bora zaidi, fanya mazoezi kwenye akaunti ya demo kwanza.

    Kwa upande mwingine, ikiwa unapata faida mara kwa mara, unaweza kufikiria kuongeza leverage yako ikiwa inafaa kwako. Exness hutoa leverage kuanzia 1:2 hadi 1:Isiyo na kikomo chini ya masharti fulani.

    Fungua Akaunti ya demo ya standard katika Exness na ufanye mazoezi ya biashara kwa kutumia leverage tofauti. Tazama jinsi ilivyo rahisi kubadilisha leverage katika Eneo la Binafsi. Mara tu unapopata leverage inayokufaa na kukuza mkakati mzuri, uko tayari kwa biashara halisi.

    Shiriki


    Anza kutrade

    Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.