Jinsi ushindi wa Trump utaathiri masoko ya kimataifa
Na Team Exness
6 Novemba 2024
Nambari zipo, na Januari hii, Donald J. Trump ataapishwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani. Ikizingatiwa kuwa sera za Trump ni tofauti sana na za Biden, ni jambo la busara kutarajia kuathirika kwa kifedha, lakini hiyo inamaanisha nini kwa traders?
Kuna mali tatu ambazo traders wengi wenye uzoefu watakuwa wakifuatilia. Tayari wanaangazia dhahabu na kutokana na kupungua kwa 20% kwa spread hivi majuzi, huu ndio wakati bora zaidi wa kutrade XAUUSD katika Exness. Litakuwa la busara pia kuzingatia kuongeza indices kama vile S&P500 na mafuta ghafi kwenye taarifa zako za soko. Hii ndiyo sababu:
Mali tatu za kuangazia
Ajenda ya kiuchumi ya Donald Trump kwa muhula wake wa pili inafafanuliwa na kupunguzwa kwa ushuru kwa kiwango kikubwa, kupunguzwa kwa udhibiti na msisitizo mkubwa kuhusu ya uhuru wa nishati.
Tunapotathmini athari zinazoweza kutokea za kiuchumi za utawala wa Donald Trump, hasa kwenye USOIL, SPX na XAUUSD, ni muhimu kuelewa sera zake za kiuchumi anazopendekeza na athari zake.
1. USOIL (Bei za Mafuta Ghafi)
Ahadi ya Trump ya kuongeza uchimbaji wa mafuta, iliyojumuishwa katika kauli mbiu yake ya ‘drill, baby, drill’, inaweza kutoa shinikizo kwa bei za mafuta.
Sera: Utawala wa Trump unaweza kupea kipaumbele kukuza uzalishaji wa mafuta ya ndani kupitia kupunguza udhibiti, kufungua ardhi zinazomilikiwa na serikali kwa uchimbaji na kutoa motisha ya ushuru kwa kampuni za nishati. Urejeshaji wa sheria za mazingira huenda ukapunguza gharama za uendeshaji za kampuni za mafuta na kuhimiza shughuli zaidi za utafutaji na uzalishaji. Mbinu hii inalingana na sera yake ya nishati ya "America First", inayolenga kupunguza utegemezi wa mafuta ya kigeni na kupunguza bei za mafuta.
Matokeo: Kuzingatia kwa Trump kwa uhuru wa nishati na kupunguza udhibiti kunaweza kusababisha ongezeko kubwa la uzalishaji wa mafuta ya ndani. Kufungua ardhi zinazomilikiwa na serikali na kuharakisha vibali vya kuchimba mafuta kunaweza kuongeza usambazaji na kusababisha bei za mafuta kushuka.
Zaidi ya hayo, sera za biashara za Trump na ushuru unaopendekezwa kwa Uchina zinaweza kuongeza mvutano wa kijiografia na kisiasa na kihistoria kusababisha volatility ya soko la mafuta. Kwa kuwa mauzo ya mafuta ghafi ya Marekani kwenda China huchukua zaidi ya 10% ya jumla ya mauzo ya nje, ushuru wa kulipiza kisasi unaweza kuathiri vibaya mauzo haya huku waagizaji wa China wakitafuta vyanzo mbadala.
2. SPX (S&P 500)
Kupunguzwa kwa ushuru na Trump kunaweza kuongeza matumizi ya watumiaji na faida za kampuni; hata hivyo, mfumuko wa bei na hatari za ukuaji zinaweza kupunguza kasi ya mwenendo wa kupanda wa SPX.
Sera: Zaidi ya kuongeza muda wa mapunguzo ya ushuru yaliyopo, Trump amependekeza kupunguzwa kwa ushuru kwa biashara ndogo na kuondoa kiasi cha juu zaidi cha $10,000 kwenye makato ya ushuru ya serikali na ya kieneo.
Mipango mingine ni pamoja na kupunguza kiwango cha ushuru wa kampuni kutoka 21% hadi 15% na kuondoa ushuru kwa faida fulani za mtaji na mapato ya biashara ndogo, yote yakilenga kuchochea uwekezaji na kukuza ukuaji wa uchumi.
Matokeo: Ushuru wa chini wa kampuni na kupunguzwa kwa udhibiti zinaweza kusababisha kuongezeka kwa ukuaji wa mapato na kusababisha bei za stock kupanda. Mipango ya Trump ya kupunguza ushuru inaweza kusababisha ongezeko la Pato la Taifa kwa 0.3% ikilinganishwa na makadirio ya kabla ya uchaguzi kufikia 2028 (mchoro wa kwanza). Sekta kama vile za kifedha, nishati na utengenezaji zinaweza kufanya kazi vizuri zaidi kutokana na sera zinazofaa za ushuru na kupunguzwa kwa mizigo ya udhibiti.
Hata hivyo, hatari kubwa kwa mtazamo huu ni kwamba mpango wa Trump unajumuisha ushuru mkali wa hadi 60% kwa uagizaji kutoka Uchina, unaolenga kulinda kazi za Marekani. Uwezekano wa kutoza ushuru mkubwa unaweza kusababisha ukosefu wa uhakika kwa soko na kusababisha mfumuko wa bei kwa kuwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zinakuwa ghali zaidi. Bloomberg Economics inakadiria ongezeko la 0.4% la mfumuko wa bei ikilinganishwa na makadirio ya kabla ya uchaguzi kufikia 2028 (Mchoro wa kwanza). Kurejea tena kwa mfumuko wa bei kunaweza kusababisha Fed kusitisha mpango wake wa kupunguza viwango vya ada na kuathiri mwenendo wa kupanda katika SPX.
Jinsi mpango wa ushuru wa Trump na Harris unaweza kuathiri bei za ukuaji
Kadirio la athari ifikapo 2028 (ikilinganishwa na athari iliyokadiriwa)
Kushoto: Pato la Taifa - Kulia: Mfumuko wa bei
Chanzo: Bloomberg Economics
Zaidi ya hayo, mfumo wa Shirika la Biashara Ulimwenguni unapendekeza kwamba ikiwa mpango kamili wa ushuru wa Trump utatekelezwa, Pato la Taifa linaweza kupungua kwa 0.8% na kuongeza bei kwa 4.3% ifikapo 2028, ikizingatiwa kuwa ni nchi ya Uchina pekee itakayolipiza kisasi.
Ikiwa nchi nyingine pia zitaweka hatua za kulipiza kisasi, athari itakuwa mbaya zaidi, huku Pato la Taifa likipungua kwa 1.3% na bei kupanda kwa 0.5% pekee, kwa kuwa kupungua kwa mauzo ya nje kunaweza kupunguza ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei (Mchoro wa pili).
Kuongezeka kwa vita vya kibiashara kutapunguza ukuaji wa Marekani, kuongeza bei.
Kadirio la athari za mipango ya ushuru ya Trump kufikia 2028 (ikilinganishwa na atahari iliyokadiriwa)
Kushoto: Ikiwa Uchina na ulimwengu wote utalipiza kisasi
Kulia: Ikiwa Uchina pekee italipiza kisasi
Chanzo: Bloomberg Economics
3. XAUUSD (Dhahabu)
Dhahabu inaweza kufaidika kutokana na kuongezeka kwa mivutano ya trade na sera za Trump za kuchochea ukuaji wa uchumi.
Sera: Trump anapanga kutekeleza ushuru wa 20% kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje na 60% kwa bidhaa za Uchina na hivyo kuongeza gharama kwa watumiaji huku akilinda viwanda vya ndani. Mkakati huu unatokana na mbinu ya "America First" na unaweza kuongeza mivutano ya kisiasa na kijiografia na kusababisha kutokuwa na uhakika wa kiuchumi.
Zaidi ya hayo, Trump anapendekeza kupanua Sheria ya Kupunguza Ushuru na Kazi, ambayo ilipunguza kiwango cha ushuru wa kampuni kutoka 35% hadi 21% na ana mipango ya kupunguza zaidi hadi 15% na kupunguza viwango vya ushuru wa mapato ya kibinafsi.
Matokeo: Muunganisho wa kupunguzwa kwa ushuru na kuongezeka kwa matumizi unaweza kusababisha kuongezeka kwa mapato yanayoweza kutumiwa na matumizi na yanaweza kusababisha kurejea kwa mfumuko wa bei, hali ambayo inaweza kufanya dhahabu kuwa hedge ya kuvutia.
Zaidi ya hayo, msimamo mkali wa Trump kuhusu ushuru na trade unaweza kuongeza mivutano ya kijiografia na kisiasa na hivyo kusababisha wawekezaji kuwekeza katika mali salama kama vile dhahabu na kusababisha bei ya dhahabu kubaki juu. Wakati wa urais wake kuanzia 2017 hadi 2021, bei ya dhahabu iliongezeka kwa zaidi ya 70%, ikichochewa na vita vya trade kati ya Marekani na Uchina na janga la COVID. Ingawa historia huenda isijirudie, mara nyingi hulingana.
Hitimisho
Huku Trump akitarajiwa kurejea kama rais wa 47, masoko yanajitayarisha kwa mwenendo unaobadilikabadilika. Mafuta, dhahabu, na S&P 500 zote ziko tayari kwa mabadiliko makubwa na fursa kwa traders ni nyingi sana. Lakini ni wale tu walio tayari kuchukua hatua haraka watakaonufaika.
Katika Exness, utapata spreads ndogo zaidi, hata wakati wa volatility iliyochochewa na Trump. Iwe unafanya trade ya dhahabu, mafuta au mali zinazohusiana na Marekani, jukwaa letu hukupa masharti yasiyoweza kulinganishwa ili kutrade kwa ujasiri. Hakuna ada, execution ya haraka na usaidizi wa kila saa—kila kitu unachohitaji ili kupata habari mapema kwenye soko hili linalobadilika haraka chini ya Trump.
Swali sio kama masoko yatabadilika Trump akiwa rais, ni mabadiliko hayo yatakuwa makubwa vipi. Usingoje hadi kuchelewa sana. Fanya trade ya athari ya Trump kushinda uchaguzi katika Exness—jiunge na traders 800k+ na unufaike zaidi kutokana na wakati huu wa kihistoria.
Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.
Mwandishi: